
Mt Meru
MASHADA HEWANI
Full mzuka! hii picha nimeikubali umeipata haswa. huku ndio kwetu tunaishi karibu na huu mlima meru. kijiji chetu kinaitwa KIMELOK village ukija tena siku nyingine nitakutembeza hadi kwenye maporomoko ya maji Wazungu wanaita waterfalls.
Umenifurahisha sana.
Tafadhali naomba tuzidi kuwasiliana tumia email adress yangu hapo juu
Translation
Full mzuka (?). I must say you really got that picture right. This is our home, we live near that Meru mountain. Our village is called KIMELOK and if you come some other day I'll show you the waterfalls.
Please let us communicate more, use the email address above.
Olparakuoni,
Hukutoa email address yako lakini. Halafu nasoali kuhusu lugha: "Mashada hewani" maana yake nini? Na "full mzuka"?




LUGHA
Mashada hewani maana yake furahaa shereee sherekea. Mashada namaanisha mashada ya maua, Mashada hewani yana pepea kwa furahaa niliyo nayo kuona mlima wa nyumbani ukionekana na kujitangaza vyema kwenye tovuti.
Full mzuka= shangwe kubwa, mzuka maana yake hisia kali ya furahaa, full mzuka furaha iliyo pitiliza kiwango kama ingekua ni kimiminiko basi kimezidi kipimo na sasa inamwagika kwa jinsi ilivyo nyingi.
Nadhani umenipata.
Naomba unieleze kuhusu wewe upo wapi na picha hii ulipiga lini?
Email adress yangu ni olparakuoni(at)gmail(dot)com